Mwenyekiti wa TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, Bi. Asha Ngoma akionyesha
cheti cha Uvumbuzi kilichotolewa na serikali mwaka 1984, mbele ya waandishi wa
habari, katikati ni Mzee Jumanne Mhero Ngoma, Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite,
Kulia ni Bw. Baraka Msuya, Mjumbe wa taasisi.
Mwenyekiti wa TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, Bi. Asha Ngoma
akikifanunua jambo kuhusu shughuli za taasisi akiwa pamoja Mzee Jumanne Mhero
Ngoma, Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite na Bw. Baraka Msuya, Mjumbe wa taasisi.
Mwenyekiti wa TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, Bi. Asha Ngoma
akionyesha cheti cha maabara ya madini
kilichotolewa mwaka 1967, mbele ya waandishi wa habari, kinachoonyesha
ni madini pekee Duniani
Asasi mpya ya kiraia inayojulikana
kwa jina la TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, kwa kifupi “TAFFO”,
Yatambulishwa rasmi mjini Dar Es Salaam, ambayo Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite ni mmoja wa
waanzilishi wake.
TAFFO ni asasi isiyo ya kiserikali
itakayojishughulisha na wachimbaji wadogo wadogo wa madini vijana, wanaofanya
shughuli za madini yote yanayopatikana ndani ya nchi yetu ya Tanzania yakiwemo
TANZANITE.
Malengo makubwa ya asasi hii ni:
·
Kuwawezesha
vijana kupata utaalam (elimu) katika sekta ya madini.
·
Kuwawezesha
kupata nyenzo za uchimbaji madini kutoka vyanzo mbali mbali ikiwemo Serikali,
mashirika ya ndani na nje ya nchi, Asasi, mabenki na Mtu mmoja mmoja
atakayeguswa na huduma za asasi hii.
·
Kuenzi na
Kuhifadhi historia ya uvumbuzi wa madini ya TANZANITE kwa faida ya vizazi vya
sasa na vijavyo.
Leo katika historia ya Tanzania tar 23/9/1967 siku kama ya leo,
miaka 46 iliyopita ndio siku ambayo yalivumbuliwa madini ya Zoisite ambayo kwa
leo yanajulikana kama “TANZANITE” yanayo patikana nchini Tanzania pekee,
duniani.
Mzee Jumanne Mhero Ngoma (Mvumbuzi) wa madini haya ya Tanzanite,
alizaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha Marwa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro
Wazazi wake walikuwa wafugaji wa Ng’ombe na mbuzi hivyo waliishi
maisha ya kuhamahama ili kupata malisho bora ya mifugo kama ilivyo hulka na
tabia za wafugaji.
Wakati akiendelea na shule ya msingi, mwaka 1952 wazazi wake walihama kutoka Hedaru na kwenda
kuishi Mererani. Mzee Jumanne Mhero Ngoma, aliweza kusafiri na wazazi wake hadi
Mererani, akaendelea na masomo yake katika shule iliyokuwa ikiitwa Town School
iliyopo Arusha mjini, ambako ilibidi akae na mjomba yake Bw. Ruben Mkali
aliyekuwa akiishi Arusha Mjini wakati huo.
Mzee Jumanne Ngoma alijiunga na kozi fupi ya madini iliyokuwa
ikitolewa na Wizara ya Madini wakati huo. Baada ya kumaliza kozi ya madini
katika ofisi ya madini Morogoro, Juni 1, 1966 alipata leseni ya madini baada ya
kuhitimu mafunzo hayo.
Siku chache baada ya kumiliki leseni ya utafiti wa madini, Mzee
Jumanne Mhero Ngoma alirejea nyumbani kwake Makanya.
Alipokuwa Makanya aliamua kuanza utafiti wake kijiji chake cha
Makanya. Mzee Ngoma aliaza shughuli za utafiti wa madini, ndipo akagundua
Madini ya Gypsum, na kuwa mtu wa kwanza aliyegundua Gypsum maeneo ya kijiji cha
Makanya, sasa hivi eneo hilo linaitwa Chang’onko
Hivyo alipopata elimu hiyo ya madini aliamua kwenda Meralani,
katika eneo la Lalouo kijiji cha Naisunyai kufanya utafiti wa yale mawe
aliyoyaona wakati anachunga mifugo ya baba yake. Mwaka Januari, 1967 aliamua
kuyapeleka mawe yale katika ofisi ya madini Moshi kwa uchunguzi. Alishauriwa na
afisa wa madini kipindi hicho Mr. Bills, ofisi ya madini Moshi itayapeleka
kwenye maabara ya taifa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Ndugu waandishi wa habari, Mnamo tarehe 23 Septemba 1967 maabara ya
Dodoma ilithibitisha kuwa ni
madini ya Zoisite ambayo kwa wakati huo hayakuwa na soko, lakini wakashauri
huenda ya kawa na soko siku zijazo.
Mnamo Mwaka 1984, serikali ya Jamhuri ya muungano ilipotambua rasmi
Mvumbuzi ya madini hayo na kuyapa jina la “TANZANITE” na kumtunukia cheti cha
uvumbuzi katika sherehe ya siku ya wafanyakazi zilizofanyika mkoani Mbeya
No comments:
Post a Comment